Kutiliwa usingizi na kuwekwea ganzi kwa ajili ya upasuaji kwa watoto na vijana

Taarifa kwa wazazi/jamii


Hapa utapata habari jinsi ilivyo kama mtoto wako atahitaji kutiliwa usingizi kwa njia ya dawa (narcosis) kwa ajili ya upasuaji, (surgery) au uchunguzi , wa ndani.

Utajulishwa juu ya maandalizi na taratibu ya kufunga kabla hamjafika hospitalini.

Tumesimulia pia, itakavyokuwa ambapo wewe na mtoto wako mtafika hospitalini,

Astrid Lindgrens Barnsjukhus, (hospitali kwa watoto na vijana) Utaratibu kwenye Wadi ya upasuaji na Wadi ya kuamshwa.

Hapa utajulishwa juu ya aina tofauti ya kutiliwa usingizi,narcosis, hatari za narcosis na utapata msaada jinsi unavyoweza kumweleza mtoto wa umri mbalimbali juu ya yale atakavyoyakuta hospitalini.

Njia nzuri kujiandaa kabla ya kwenda hospitalini ni kusoma wanavyosimulia wengine, kwa hiyo tumeorodhesha vitabu vinavyofaa kwa wazazi na kwa watoto.

Kama utakuwa na maswali mengine ingawa umesoma taarifa yetu, ni vizuri kuziandika ili ukumbuke kutuuliza tutakapoonana hospitalini.

Salamu kutoka wafanyakazi wanaoshugulika na narcosis

Wadi/section ya narcosis kwa watoto, Astrid Lindgrens Barnsjukhus

//Search

twitter icon

Astrid Lindgren ChildrenĀ“s Hospital |Ā Karolinska University Hospital 171 76 Stockholm


© Karolinska University Hospital

mail
Logotype